Jumanne, 1 Aprili 2014

MAAMBUKIZI YA VVU YAZIDI KUPUNGUA NCHINI

Fatuma_Mrisho-March31-2014_1350b.jpg
Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), Dk. Fatuma Mrisho.
 

Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) yanazidi kupungua mwaka hadi mwaka nchini. Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), Dk. Fatuma Mrisho wakati akifungua semina kwa mahakimu, maofisa wa polisi na wanasheria wa Serikali wa mikoa ya Dae es Salaam, Pwani na Morogoro

Dk. Mrisho alisema takwimu zinaonyesha kuwa maambukuzi ya ukimwi yamepungua kwa kiasi kikubwa nchini.

Alisema takwimu zinaonyesha kuwa kuwa Tanzania Bara na Visiwani kuanzia mwaka 2003 hadi 2004 maambukizi hayo yalikuwa ni asilimia 7.

Mwaka 2007 hadi 2008 yalishuka mpaka kufikia asilimia 5.7 na mwaka 2011 hadi 2012 yalishuka zaidi hadi kufikia asilimia 5.1 kwa kiwango cha kitaifa.

Tanzani Bara pekee kiwango cha maambukizi ya VVU ni asilimia 5.3 zaidi ya kiwango cha kitaifa.

"Kila mtu kwa namna moja au nyingine anaguswa na ukimwi maana hakuna ukoo, kijiji, wilaya na mkoa usio na mtu anayeishi na VVU na hivyo hadi nchi nzima inaguswa na hali hiyo, " alisema Dk.. Mrisho.

Aliwaasa washiriki hao wa semina na Watanzania kuacha ngono zembe ili maambukizi ya ukimwi yaweze kupungua na kufikia kiwango cha asilimia sifuri hadi kufikia mwaka 2015.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni