Habari kutoka ndani ya chama tawala cha serikali ya Zimbabwe zinasema kuwa kiongozi wa muda mrefu na rais wa taifa hilo la Afrika, Robert Mugabe amezirai ghafla.
Happyton Bonyongwe, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Zimbabwe aliripotiwa akisema kwamba ulinzi umeimarishwa katika ikulu ya Zimbabwe, siku moja baada ya hofu ya kuzirai kwa Mugabe na hali yake yake ya kiafya kuenea nchi nzima.(HD)
Baba Jukwa, ambaye ni mtoa taarifa ndania ya chama tawala cha Zanu-PF ambaye anatumia mtandao wa facebook ameandika kuwa rushwa na ufisadi katika serikali ya Mugabe vimekithiri huku taarifa ya kuanguka na kuzirai kwa Mugabe zikiwa zimezagaa nchi nzima.
Hata hivyo, aliongeza kuwa Rais Mugabe hali yake ya kiafya si nzuri lakini katibu wa Rais huyo ndugu George Charamba, alikanusha taarifa hizo kwamba Mugabe ni mgonjwa.
Kumekuwa na uvumi kwa miaka kadhaa kwamba Rais Mugabe , ambaye anafikisha umri wa miaka 90 mwezi ujao, ana kansa ya kibofu.
Baba Jukwa , ambaye anajiita " disgrunteld Zanu- PF " , alisema siku ya Jumamosi kuwa Rais Mugabe alikuwa " kwenye ziara yake ya mwisho kwenye sehemu kadhaa nchini Zimbabwe na madaktari wake walimshauri apumzike.
Baba Jukwa amesema kwamba mafanikio katika mapambano ya rushwa ni safari ndefu na kwamba panahitajika uwazi katika Zimbabwe. Katika siku za nyuma, Mugabe alionya kuwa Edward Chininga mwanachama wa zamani wa Zanu- PF na mbunge ambaye alikuwa mtu muhimu kwa Mugabe, atakufa hivi karibuni.
Majuma kadhaa baadaye, Mr Chininga alikufa katika ajali ya gari. Ajali za barabarani ni mfumo wa kawaida mauaji katika Zimbabwe.
Katika ujumbe wake wa karibuni, Baba Jukwa anasema kwamba usalama umekuwa imara Ikulu lakini hakuna taarifa juu ya Bw. Mugabe kuwa yuko wapi.
"Kama ni kweli kwamba yeye (Mugabe) amekufa, uwezekano ni wa kuweka mwili wake kwenye jokofu hadi wakuu wa usalama watakapopita na kutangaza rasmi, " Baba Jukwa alisema.
"Wakati huo huo, wananchi wa Zimbabwe wameomba kuanza maombi maalum kuomba kwa ajili ya nchi yao na rais ili nchi isingiie kwenye umwagaji wa damu. "
Na.MOblog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni