ABUBAKAR SHARRIF aka MAKABURI ambaye ni mhubiri maarufu nchini KENYA ameuawa mjini Mombasa ambaye anashutumiwa kuliunga mkono kundi la Al Shaabab ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mombasa.
Abubakar Sharif aka Makaburi enzi za uhai wake
Kwa mujibu wa mashuhuda waliohajiwa na waandishi wa habari walidai kuwa mwili huo wameuokota ukiwa na majeraha ya risasi. Mashuhuda wengine walisema kuwa jana saa 12.30 akiwa na wenzake watano wakiwa wanasubiri basi ilikuja gari ndogo ambaayo ilibeba watu waliovaa kanzu nyeupe ambapo waliwashambulia kwa risasi na kuondoka mbio kuelekea mjini Mombasa.
Shehe huyo alisadikiwa kuongoza kundi la Al Hirja ambalo liko Kenya, Tanzania na Burundi. Kundi hilo pia linasadikiwa ndilo lililofanya ,ashambulizi katika kanisa moja mjini Mombasa hivi karibuni.
Aidha vurugu kubwa zimeripotiwa mjini Mombasa ambapo wafuasi wake wanasadikiwa kuanzisha fujo hizo(TK).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni