Watu wawili wamekamatwa baada ya kupatikana wakiwa na
maguruneti mawili nyumbani mwao wakati polisi wakiendelea na msako mkali mtaani
Easteligh nchini Kenya.
Wawili hao, Mume na mkewe walikuwa nyumbani wakati polisi walipopata habari
kuwahusu na vifaa walivyomiliki.
Mume mwenye umri wa miaka 60 inaarifiwa aliwauzia vijana vilipuzi ambavyo
walitumia kwa mashambulizi mjini Mombasa karibu wiki mbili zilizopita.
Polisi wamekuwa wakifanya msako katika mtaa huo wa Easteligh tangu
mashambulizi ya maguruneti kuwaua watu 6 Jumatatu usiku na kuwajeruhi wengine
30.
Mkuu wa polisi alisema kuwa wawili hao walikamatwa pamoja na watu wengine 400
katika eneo hilo huku msako wa polisi ukiendelea.
Polisi wanasema kuwa wanawahoji wawili hao kuona ikiwa wanaweza kupata
taarifa zaidi
Takriban watu 657 walikamatwa na polisi Jumatatu usiku mtaani Eastleigh,
baada ya shambulizi la kigaidi dhidi ya mkahawa kuwaua watu sita (TK).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni