Shambulio dhidi ya makao makuu ya idara ya usalama ya Somalia
mjini Mogadishu limeuwa watu 10.
Wakuu walisema saba kati ya hao ni wapiganaji wa al-Shabaab ambao waliingiza
kwa nguvu gari lilojaa mabomu katika uwa wa jengo hilo ambalo lina ulinzi
mkali.Tena washambuliaji walijaribu kuingia ndani ya jengo.
Al-Shabaab ilisema ilifanikiwa kuwaachilia huru wafungwa wengi katika makao makuu hayo, ambayo yana gereza chini kwenye handaki na pahala pa kuhoji wafungwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni