Jumatatu, 28 Agosti 2017
MAYWEATHER AMDUNDA McGREGOR
Bondia maarufu duniani Floyd Mayweather amemdunda kwa TKO Bondia Conor McGregor katika raundi ya 10 katika mpambano wa raundi 12 usiokuwa wa ubingwa. Pambano hilo lililoitwa pambano la fedha Mayweather atanyinyakulia kitita cha zaidi ya dola milioni 100 wakati McGregor atanyinyakulia kitita cha zaidi ya dola milioni 30. Pambano lilifanyika katika usiku wa kuamkia tarehe 27/8/2017 huko Marekani.
Bondia McGregor alikuwa na tambo nyingi kuwa angeshinda kwa TKO raunsi za mwanzo kabisa lakini mambo hayakuwa hivyo.
Mayweather alisema kuwa amefurahishwa na kupata mpinzani ambaye alimpa changamoto kubwa.
McGregor alianza pambano hilo kwa kuongoza raundi tatu za mwanzo na Mayweather akashinda raundi ya 4 hadi ya 9 na raundi ya 10 refarii alisimamisha pambano baada ya McGregor kuzidiwa vibaya.
Mayweather amejiwekea rekodi ya mapambano 50 bila kuhindwa na ametangaza kustaafu rasmi masumbwi.
Wakati huo huo McGregor naye amesema anafikiria kuachana na ndondi ili kurejea kwenye mieleka.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni