Alhamisi, 26 Juni 2014

WATU ZAIDI YA 20 WAUAWA KWA BOMU NIGERIA

Nigeria blast (© AP Photo/Olamikan Gbemiga)
Askari wa Nigeria wa kwenye eneo la tukio

Kumetokea mlipuko mkubwa wa bomu ambalo lililenga mamia ya watu waliokuwa wanafanya manunuzi kwenye maeneo ya maduka makubwa (shopping mall) mjini Abuja. Hakuna aliyekiri kuhusika na mlipuko huo ila inasadikiwa kundi la kigaidi la Boko Haram linahusika na mashambulizi hayo.

Polisi mjini Abuja wamekiri kutokea kwa mlipuko huo na wanasema watu zaidi ya 20 wameuawa papo hapo na wengine wengi kujeruhiwa. (TK)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni