Waziri
wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akiwaeleza wafanya biashara kuendelea
kutoa ushirikiano, utakaojenga uhusiano wa kudumu kati yao na Serikali
kwa maslahi na maendeleo ya Taifa, wakati akitoa Taarifa ya muafaka
uliofikiwa kati ya wafanyabiashara na serikali juu ya Matumizi ya
Mashine za kielektroniki (EFDs) leo Jijini Dar es Salaam.
2-
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade akimshukuru
Waziri wa Fedha kwa ushirikiano wanaoendelea kuuonyesha kwa mamlaka
hiyo hasa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika suala la
ukusanyaji Kodi nchini.
3-
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabishara Bw. Johnson Minja akimueleza
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum kuridhishwa na utendaji wa
serikali katika utatuzi wa changamoto za wafanyabiashara na kuahidi
kuendelea kutoa ushirikiano ili kwa pamoja waweze kufikia malengo ya
taifa ya kuwa na uchumi imara kupitia ukusanyaji wa Kodi.
4-
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mzee Benard
Mchomvu akipongeza kazi iliyofanywa Kamati ya uhamasishaji wa matumizi ya
mashine za kielektroniki(EFDs) na kuwaasa kuendelea kutoa ushirikiano
kwa maslahi ya Taifa kwa Ujumla.
Waziri
wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akiwa katika picha ya pamoja
wafanyabiashara alipotoa Taarifa ya muafaka uliofikiwa kati ya
wafanyabiashara na serikali juu ya Matumizi ya Mashine za kielektroniki
(EFDs) leo Jijini Dar es Salaam, Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Jumuiya
ya wafanyabishara Bw. Johnson Minja na Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi
ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mzee Benard Mchomvu.
Na Anitha Jonas – MAELEZO.
Serikali yafikia muafaka katika mgogoro wake na wafanyabiashara juu ya matumizi ya mashine za kieletroniniki EFD’s.
Hayo
ameyasema jana Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya alipokuwa akitoa taarifa
hiyo kwa vyombo vya habari juu ya Serikali kufikia muafaka wa
makubaliano yaliyofanyika kwa ushirikiano wa Kamati kuu ya Taifa
iliyoshirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na
Viongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara katika ngazi ya Taifa.
“Matumizi
ya mashine za EFD yalipoanza yalileta changamoto kwa wafanyabiashara, hivyo niliunda kamati ya kitaifa pamoja na kamati katika ngazi za Mikoa
na Wilaya pamoja na wenyeviti wakuu wa mikoa kutafuta suluhu la suala
hili”alisema Mhe. Mkuya.
Waziri
Mkuya aliendelea kusema Kamati imetoa mapendekezo mbalimbali kwa
Serikali ikiwemo ya muda mfupi ambayo wameshaanza kuyafanyia kazi na
mengine ni ya kisera ambayo yatahitaji muda mrefu yatafuata utaratibu
unaopaswa katika utekelezaji wake, kwa ufuatiliaji na ushirikiano wa
karibu, kupitia kamati ya Kitaifa itakayodumu kwa kipindi cha miaka
miwili.
Naye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini Bw. Johnson Minja
aliipongeza serikali kwa kukubali kukaa meza moja na wafanyabiashara
katika kutatua mgogoro huo uliyokuwepo katika matumizi ya mashine za EFD
na kukubali kupokea changamoto za wafanyabiashara na kuahidi
kuzifanyia kazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni