Mbunge
wa Mtama, Nape Nnauye ameuliza serikali imefikia wapi kutafuta soko la
Mbaazi baada ya msimu uliopita matatizo ya soko kushusha bei kutoka Tshs 2,000 mpaka 150. Amesema serikali iliahidi Bungeni kuwa itahakikisha inahangaika kupata soko la kuaminika la zao hilo.
Nape
amesema sasa ni msimu wa kilimo hicho, kama bado hali haieleweki
wananchi washauriwe waachane na mbaazi na badala yake wajikite kwenye
mazao mengine ambayo yana soko la uhakika.
Akijibu
swali hilo naibu waziri wa kilimo, Eng. Stella Manyanya amemjibu kuwa
ni kweli hakukuwa na hali inayoridhisha kwenye soko la mbaazi na ni
kutokana na wadau waliokuwa wanategemewa sana ilikuwa ni India.
Eng.
Stella amesema mbaazi ni chakula kizuri chenye protini na watanzania
wanaweza kula badala ya kuwategemea watu wa maeneo mengine.
Amesema
biashara ni ushindani na kila watu wanahakikisha wanakidhi soko lao la
ndani, upande wa Tanzania wanaendelea kutafuta soko lakini wakati huo
huo wanaendelea kusisitiza watu wapende kutumia mbaazi.
Amesema
Dodoma Mbaazi inauzwa mpaka 1,800 kwa kilo na soko la Dar es Salaam
kwenye supermarket inauzwa mpaka 2,400 hivyo tusitegemee soko mpaka
kutoka nje kwani hata ndani ya nchi bado kuna watu wanaweza kula mbaazi
yeye akiwa mmojawapo pia inategemewa hata mashule yanaweza kutumia
wakati masoko yanaendelea kutafutwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni