Mtalii mmoja kutoka
nchini Ufaransa aliyechukua hatua za haraka amesifiwa baada ya kulizuia
basi kupingirika chini ya mteremko katika milima ya Alps nchini Austria
baada dereva wa abasi hilo kuzimia.
Gari hilo lilikuwa likipitia eneo la milima likiwa na abiria 21 wakati dereva mwenye umri wa miaka 76 alipozimia ghafla.Wakati basi lilikuwa likielekea chini ya mlima raia huyo wa Ufaransa alifanikiwa kukanyaga breki.
Basi hilo liligonga kizuizi kando ya barabara kisha likasimama. Watu wanne walipelekwa hosptalini kwa matibabu baada ya kupata mshtuko.
Abiria raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 65 aliyekuwa ameketi kando mwa dereva wakati alipozimia ghafla karibu na mji wa Schwaz magharibi mwa Austria siku ya Jumamosi.
Alitoka kwa kiti chake wakati gari hilo lilikuwa linagonga kuzuizi cha mti kilicho kando ya barabara na kukanyaga breki.
Mwaka 2004 watalii watano waliuawa wakati basi liliacha barabara na kupinduka chini ya mlima karibu ni kijiji cha Bad Dürrnberg nchini Austria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni