Jumapili, 2 Februari 2014

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA MOROGORO KUMPA POLE YA MAFURIKO


Kamanda wa kanda maalumu ya kipolisi ya Dar es Salaam Suleiman Kova akisalimiana na Rumin Shar kutoka kampuni ya Pan Africa Enterprises Ltd baada ya Kampuni yao kutoa magodoro 200 aina ya Comfy kwa ajiri ya ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea wiki iliyopita eneo la Dakawa mkoani humo na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kuwaacha mamia bila makazi

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joe Bendera akimweleza kwa kina hali ilivyokuwa baada ya kutokea kwa mafuriko Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq. Nyuma katika picha ni sem trela tano zilizokuwa zimepakia vifaa na vyakula

Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadiq akimshukuru mmoja wa wafanyabiashara wa Mkoa wa Dar es Salaam Rumin Shar kutoka kampuni ya Pan Africa Enterprises Ltd baada ya Kampuni yao kutoa magodoro 200 aina ya Comfy kwa ajiri ya ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea wiki iliyopita eneo la Dakawa mkoani humo na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kuwaacha mamia bila makazi

Waathirika wa mafuriko ya dumila wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq hayuko kwenye picha alipotembelewa leo

Mkurugenzi wa Home Shopping Centre Gharib Said Mohammed (GSM) kushoto akitembea na Mku wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meki Sadiq katika daraja lilosababisha watu wa kutoka Dar kwenda Dodoma kusimama kwa muda

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni