Vurugu kubwa zilizuka jana jioni kwenye msikiti huko Mombasa ambapo watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa. Aidha kuna tetesi kuwa kuna vifo kadhaa. (tunaomba radhi baadhi ya picha sio nzuri)
Askari akijihami wakati wa vurugu kubwa zilizozuka jana majira ya jioni Jiji la Mombasa wakati Waumini wa dini ya Kiislamu wa Msikiti 'Masjid Mussa' ambapo waumini hao wamedaiwa kuwa walikuwa wameandaa mkutano wa hadhara waliouita Kongamano ambao Serikali ilikataa kutokuwepo kwa muhadhara huo na wao kupinga maamuzi hayo.
Imeelezwa kuwa Baada ya kukatazwa kufanya muhadhara huo, waliamua kuweka Bendera ya Kiislamu katika Msikiti huo huku wakitoa 'Fatwa' kuwa kuanzia leo hawaitambui Bendera ya Kenya, jambo ambalo lilipelekea kutokea kwa vurugu hizo baina ya Askari na waumini hao. Aidha imeripotiwa kuwa watu kadhaa wamefariki dunia katika vurugu hizo na wengine kujeruhiwa.
Askari wakilinda moja ya mtaa unaoelekea Msikitini hapo.
Taswira ya msikiti huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni