Upigaji kura ya maoni unakaribia kuanza Scotland kwa raia wa nchi hiyo kuamua kujitenga au kubaki kwenye himaya ya Uingereza.
Hiyo ni kura ya maoni ya kihistoria kwa nchi hiyo iliyokuwa kwenye muungano wa Uingereza miaka 307 iliyopita.
Kiongozi wa Scotish National Party, Alex Salmond, ametaja kampeni ya kuitisha Uhuru wa Scotland kutoka kwa Uingereza kama tukio muhimu zaidi la kidemokrasia kuwahi kutendeka nchini humo, na ambalo amesema tayari limebadilisha mfumo wa maisha eneo la Scotland.
Idadi kubwa ya wapiga kura wamesajiliwa na kwa mara ya kwanza vijana wenye umri wa miaka 16 na 17 wataruhusiwa kupiga kura.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni