Mwanamume
mmoja mwenye asili ya nchini Mali ambaye aliwaficha wauza maduka katika
duka kubwa maarufu kama supermarket mjini Paris wakati wa shambulio la
kigaidi lililotekelezwa na watu wanaodhaniwa wapiganaji wa kiislamu
amepewa hati halali ya ukaazi na kuwa raia halali wa Ufaransa.
Kwa
pamoja waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls na waziri wa mambo ya ndani
Bernard Cazeneuve walizungumza katika karamu ya kumpongeza na
kumshukuru Lassana Bathily kwa ushujaa wake kwa niaba ya taifa lake .Kijana huyo ana umri wa miaka ishirini na minne, na kazi aifanyayo ni muuzaji msaidizi katika supermarket hiyo,ambaye alifanya kazi kubwa ya kuwaongoza na kuwaficha katika eneo la juu la chumba cha baridi cha kuhifadhia bidhaa na kisha akazima taa za duka hilo kubwa, kisha akawapigia polisi simu kwa msaada wakati walipovamiwa.
Baada ya tukio hilo, likapitishwa azimio aitwe apewe uraia wa nchi hiyo ya Ufaransa, hata hivyo inaelezwa kwamba Bathily ameishi nchini humo kwa miaka tisa sasa na alikuwa ameshaomba ridhaa ya kuwa raia halali wa nchi hiyo mwaka wa jana.
Wakati wa uvamizi huo, Amedy Coulibaly,aliwaua watu wanne wenye asili ya Uyahudi katika duka hilo kubwa kabla hajapigwa risasi na polisi na kufa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni