Jumatano, 21 Januari 2015

ZITO ATOA KAULI KUHUSU KUREJEA CHADEMA

zito

Mheshimiwa Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini mwanzoni mwa mwaka 2014 alikuwa na mgogoro mkubwa na Chama chake cha Chadema. 
Magazeti yaliyotoka siku chache zilizopita yaliripoti taarifa ya Mbunge Zitto Kabwe kurudi tena Chadema na hiki ndicho alichokisema Zitto Kabwe. 
Swali lilikuwa ni yeye kuhusu kurudi Chadema
’Hapana nadhani hizo ni tetesi kwa sababu sijatoa kauli yoyote kuhusiana na hilo na moja mimi bado mwanachama wa Chadema kwa sababu nina kesi mahakamani na kesi hiyo haijaamuliwa bado inaendelea’
‘Sijawahi kutoka kwenye uanachama wa Chadema, mtu anaposema nataka kurudi Chadema hayuko sahihi, inafahamika nilikuwa na matatizo na chama hatujaweza kuyatatua, hakuna mazungumzo yoyote ambayo yamefanyika lakini kuna baadhi ya watu wameanza kuleta hayo mazungumzo’.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni