Jumanne, 14 Oktoba 2014

BURIANI PROFESA MAZRUI

Profesa Ali Mazrui enzi za uhai wake.
MSOMI mashuhuri wa masuala ya kisiasa, utamaduni wa Kiafrika na dini ya kiisilamu wa nchini Kenya, Profesa Ali Mazrui ameaga dunia jana akiwa Marekani.
Profesa Mazrui enzi za uhai wake
Mazrui alyekuwa anaishi nchini Marekani, amefariki akiwa na umri wa miaka 81 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Taarifa zinadai kuwa Profesa Mazrui atazikwa mjini Mombasa, Pwani ya Kenya alikozaliwa.
Enzi za uhai wake, marehemu alitoa ombi la kutaka kuzikwa Mombasa akisema angependa kuzikwa katika jumba la kihistoria la Fort Jesus.
Kabla ya kifo chake, Marehemu Mazrui alikuwa anafundisha katika Chuo Kikuu cha Binghamton mjini New York, Marekani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni