Jumanne, 15 Aprili 2014

KAULI ZILIZOTOLEWA BUNGENI NA TUNDU LISSU, WASSIRA, MTIKILA NA ISMAIL JUSSA


Zifuatazo ni kauli zilizotolewa na viongozi mbalimbali wa zile kamati kwenye bunge la katiba linaloendelea sasa hivi hapa Dodoma ambapo viongozi hawa leo April 14 2014 wameendelea kuwasilisha taarifa kutoka kwenye kamati zao,
Ni maoni ya pande mbili ambazo ni maoni ya wengi ambao ndio wanaounga mkono serikali mbili alafu maoni ya wachache ambao wanaunga mkono uwepo wa serikali tatu.


Tundu Lissu: ‘Nusu karne ya uongo iishe, Tanganyika iliuawa na amri za Mwalimu Nyerere na hakuwa na mamlaka kisheria kuiua, hatujawahi kuwa nchi moja, habari ya Tanzania kuwa nchi moja iliingizwa ktk katiba miaka 20 baada ya muungano, nchi hii ni haramu…. miaka 50 ya kudanganyana ikome, nchi hii inahitaji kuelezwa ukweli’
Mchungaji Mtikila: ‘tulijengwa kwenye misingi ya uongo ndio maana Mungu alishindwa kubariki hii nchi yetu kwa miaka 50, uongo tuuondoe, suala la muungano lilikuwa utapeli wa kisiasa, tuurudie ukweli kuhusu uhuru wa Watanganyika na Wazanzibari’
Mh Wassira: ‘Hati ya Muungano ipo, naahidi kwa niaba ya Jamuhuri itawasilishwa kwa Mwenyekiti ndani ya siku mbili zijazo, kama Wananchi wangetoa maoni kutaka kuvunja muungano, je tume ingeyaleta? serikali 3 italeta mgongano’
Mh Wassira: ‘Katiba ya Zanzibar ndiyo itabakia kuwa sheria kuu kwa Zanzibar kwa mambo yasiyokuwa ya muungano, tukiweka serikali 3 hapa zikaweka masharti kuna watu watapata matatizo, itapunguzia Wazanzibari fursa’

Ismail Jussa: ‘Hoja za historia kwamba tulikuwa vipi haziwezi kulibakisha taifa katika mgando, ukiangalia katiba ya muda ya mwaka 1965 inaendelea kuitambua Tanganyika na kuwepo makamu wawili wa Rais’
‘Mkataba wa muungano haukutoa mamlaka kwa chombo chochote kubadilisha kilichopo ndani, ajabu bunge limefanya, tunapokuwa Zanzibar tunasema mengine tukija huku tunaufyata, Wazanzibari watatuhukumu’
Zanzibar tumeachwa watupu, tumechoka na hatukubali tena, ktk mfumo wa serikali mbili Zanzibar haitaweza kujisimamia kamwe, hatutakubali kuendelea nao
Ismail Jussa: ‘Kama kuna nia njema kwa nini kuna kufichaficha, mfano mwingine hai ni Rais wa Zanzibar kuondolewa kuwa makamu wa Rais (TK)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni