Wafanyakazi 2 raia wa Kenya wa mashirika ya misaada ya kibinadamu
ambao walikuwa wametekwa na wapinaji wa kiislamu wa Al shabaab mwaka 2011
wameokolewa na majeshi ya Kenya.
Daniel Njuguna ambaye alikuwa akifanya kazi katika shirika la Madaktari wasio
na mipaka Medecins Sans Frontieres MSF na James Kiarie wa Shirika la Care
International, walichunguzwa afya zao na walitarajiwa kusafirishwa kwenda
Nairobi.
Awali walikuwa chini ya uangalizi wa majeshi ya Kenya ambalo lipo kwenye
kikosi cha Umoja wa Afrika kilichopo nchini Somalia AMISOM.
Kenya ilituma majeshi yake kwenda nchini Somalia mwaka 2011 kujiunga na
AMISOM kufuatia matukio ya utekaji nyara yaliyokuwa yakiendeshwa na wapiganaji
wa Al shabaab katika mipaka ya nchi hiyo na Somalia.
Majeshi ya AMISOM yakishirikiana majeshi yale ya serikali ya Somalia yamekuwa
yakiendesha mapambano dhidi ya wapiganaji wa Al Shabaab Wanajeshi wa Kenya waliopo AMISOMambao wanafadhiliwa na
kundi la kigaidi la al Qaeda linaloshikilia maeneo ya kusini na katikati mwa
Somalia (TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni