Mshindi wa tuzo la
malkia wa urembo wa Uturuki 2017 amepokonywa taji hilo baada ya mojawapo
ya machapisho yake ya mtandao wa Twitter kufichuliwa.
Itir Esen
mwenye umri wa miaka 18 alilitaja jaribio la mapinduzi ya mwaka uliopita
nchini humo na kufananisha damu iliomwagika kutukokana na hedhi yake.Waandalizi wa shindano hilo walisema kuwa chapisho hilo halikubaliki na kuthibitisha uamuzi wao wa kumpokonya taji hilo saa chache tu baada ya kupata ushindi.
Hata hivyo bi Esen amesema kupitia mtandao wake wa Instagram kwamba chapisho hilo silo la kisiasa.
Chapisho hilo lilichapishwa wakati wa maadhimisho ya mapinduzi hayo manmo tarehe 15 mwezi Julai wakati ambapo takriban watu 250 walifariki wakikabiliana na jaribio hilo la mapinduzi lililotekelezwa na upande mmoja wa jeshi.
Aliandika: Nimepata hedhi yangu asubuhi ya leo kusherehekea watu waliopoteza maisha yao mnamo mwezi Julai Ninasherehekea siku hiyo kwa kuvuja damu ya watu waliopoteza maisha yao.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekuwa akiwaita ''mashahidi'' watu waliofariki wakipinga mapinduzi hayo.
Waandalizi wa shindano hilo wanasema kuwa hawakuliona chapisho hilo hadi baada ya shindano hilo siku ya Alhamisi mjini Instabul ambapo walifanya mkutano kulijadili kabla ya kuapata uamuzi huo.
Bi Esen sio mshindi wa kwanza kupokwa taji hilo nchini Uturuki.
Mwaka 2016, mshindi mwengine wa taji hilo bi Merve Buyuksarac, alipewa hukumu ya jela ya miezi 14 kwa kumtusi rais Erdogan katika shahiri la kejeli alilolichapisha katika mtandao wa kijamii.
Bi Buyuksarac ambaye alishinda taji hilo 2006 pia alizuiwa kwa muda kuhusu chapisho hilo 2015.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni