Jumanne, 26 Septemba 2017

Wanandoa waliokamatwa Urusi wamekiri kuua watu 30

Generic shot of Krasnodar

 Mji wa Krasnodar umeshangazwa sana na tukio hili

Wanandoa waliokamatwa kwenye mji ulio kusini magharibi mwa Urusi wa Krasnodar, wamekiri kuwaua hadi watu 30.
Dmitry Baksheev, 35, na mke wake Natalia, walikamatwa baada ya mwili uliokuwa umekatwakatwa ulipopatikana kwenye kambi ya jeshi ambapo wawili walikuwa wanaishi.
Polisi walithibitisha kuwa bidhaa kadhaa za chakula na nyama vilivyopatikana nyumbani kwao vinachunguzwa ikiwa vina vinasaba (DNA) vya binadamu.
Simu ya mkononi iliyookotwa na wajenzi wa barabara mapema mwezi huu ikiwa na picha za miili iliyokuwa imekatwakatwa ndiyo ilikuwa chanzo cha kugundulika uhalifu huu.
Picha moja ilyochapishwa na vyombo vya habari nchini Urusi ilimuonyesha Bw Baksheev akiwa na  sehemu ya mwili wa binadamu kwenye mdomo wake jambo lililoashiria kuwa walikuwa wakila nyama ya binadamu.
Mwili wa mwanamke mwenye umri wa miaka 35 kisha uliripotiwa kupatikana katika chuo cha kijeshi ambapo wawili hao wanaishi.
Mwili huo ulikuwa umekatwakatwa na mkoba ulio na mali za muathiriwa nao ulipatikana.
Wizara ya mambo ya ndani nchini Urusi ilithibitisha kuwa mwanamume aliye kwenye picha hizo ametambuliwa na kukamatwa.
Picha zimetolewa kwa vyombo vya habari nchini Urusi zinazoripotiwa kuonesha polisi wakipekua nyumba ya wawili hao.
Vipande kadhaa vya miili ya binadamu vilioneshwa kwenye picha huku vingine vikiwa ndani ya ndoo.
Vyombo vya habari vinasema kuwa picha zilizopatikana zimechapishwa kwenye ukuta na kwenye simu zilionesha kuwa mauaji hayo huenda yalianza karibu miongo miwili iliyopita.
Picha moja ni ya tarehe 28 Disemba mwaka 1999 na inaonyesha kichwa cha binadamu kikiwa kwenye sahani pamoja na tunda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni