Wasichana waliochaguliwa kunufaika na Mpango huo wakiwa Katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser
Shear
Illusions inasherehekea mwongo mmoja wa urembo nchini Tanzania kwa kuzindua
vipodozi vyake ijulikanayo kama LuvTouch Manjano!
Uzinduzi
huu utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kwenye Ukumbi wa Diamond
Jubilee VIP Hall. Shamrashamra hizi pia itatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa
kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua
kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia vipodozi.
Mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na mtoa mada mkuu atakuwa
ni Balozi Mwanaidi Majaar.
Shear
Illusions, imeweza kutambulisha urembo na muonekano wa mwanamke wa kitanzania
kwa Zaidi ya miaka kumi. Wamebaisha urembo kuanzia kujipodoa, nywele, vipodozi
na vito hadi blog na jarida inayoelezea masuala ya urembo. Baada ya kuuza
bidhaa mbali mbali ya urembo toka nchi mbali mbali, Shear Illusions inazindua
rasmi bidhaa yake ya LuvTouch Manjano.
LuvTouch
Manjano ni maalum kwa ajili ya kumpendezesha mwanamke wa kitanzania. Kuna aina
kumi ya vipodozi msingi kuanzia Mwanzi na Mpodo hadi kahawa na ardhi. Bidhaa
hizi zimezingatia hali ya hewa ya joto. Vipodozi hivi vinalengo la kuongeza
muonekano wako kwa hali yoyote.
Shear Illusions inazishukuru kampuni zifuatazo waliojitokeza kusaidia hafla hii ya kuwawezesha
wanawake; NSSF, TCRA, Clouds Media, Maxcom, A1 Outdoor, Mr. Price, Cassandra
Lingerie, Amina Design, Maznat Bridal, Advertising Dar, Beauty Point, Hugo
Domingo, I-View Media, FAIDIKA, Benchmark Productions, Fasta Fasta, TENSHI,
Jardin Modeling Agency na mashirika mbali mbali Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha
Nasser Katikati akiongea na Vyombo vya Habari leo wakati akelezea
Mandalizi ya Uzinduzi wa Manjano Foundation Ambao ni Mpango unaolenga
kuwawezesha Kutoa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Wasichana wa
Kitanzania.Mpango Uzinduzi
huu
utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kuanzia saa 6 mchana kwenye Ukumbi wa
Diamond
Jubilee VIP Hall. Utatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa
kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua
kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia
vipodozi. Mgeni Rasmi anategemewa Kuwa Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu
Pinda
Meneja Mradi wa Manjano Foundation Mama Gugu
Ndolvu Akieleza jambo leo wakati wakiongea na wanahabari kuhusu Mradi
huo ambao ni Mkombozi kwa wakinamama wasio na Ajira Akiwa samabamba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser Pamoja na Aunty Sadaka Gandi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni