Viongozi
Kaskazini mwa Kenya wamesema kuwa wapiganaji wa kundi la kigaidi kutoka
Somalia la Al Shaabab waliuvamia msikiti mmoja katika kaunti ya Garissa
kwa masaa kadhaa.
Wapiganaji hao waliwahutubia waumini waliokuwa msikitini kwa karibu saa mbili kabla ya kutokomea mwituni.Waliikosoa serikali ya Kenya na kuonya waumini dhidi ya kuwa majasusi wa serikali ya Kenya.
Mwezi uliopita Al Shaabab walivamia chuo kikuu cha Garissa na kuwaua watu 150 wengi wao wanafunzi.
Kundi hilo kutoka Somalia linaaminika kuwa na wafuasi nchini Kenya ambapo limetekeleza mashambulizi kadha katika jitihada ya kuilazimisha serikali ya Kenya kuondoa majeshi yake nchini Somalia.
Majeshi ya Kenya ni miongoni mwa kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Afrika Amisom ambao wanaisaidia serikali dhaifu ya Somalia kupigana na waasi wa Al Shabaab.
Msikiti huo upo takriban kilomita 40km kutoka mji wa Garissa kulikotokea shambulizi la chuo kikuu mwezi uliopita
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni