Jumamosi, 16 Mei 2015

ALIYESHAMBULIA BOSTON AHUKUMIWA KIFO

 
Dzhokhar Tsarnaevaliyeshambulia Boston
 
Dzhokhar Tsarnaev ambaye alikamatwa kutokana na mashambulizi ya Boston amehukumiwa kifo.  

Meya wa mji wa Boston Martin Walsh amesema kuwa ana matumaini kuwa hukumu ya kifo aliyopewa mshambuliaji kwenye mbio za Boston Marathon itawapa nafuu wale wote walioathiriwa na shambulizi hilo.

Iliwachukua majaji saa 14 kuamua ikiwa Dzhokhar Tsarnaev atauawa kwa kudungwa sindano ya sumu badala ya kupewa kifungo cha maisha.

Waathiriwa kadhaa walielezea kuridhika kwao wakisema kuwa uamuzi huo utawawezesha kuendelea na maisha yao.

Wengi wanahofu kuwa ikiwa rufaa itakatwa, itawaongezea machungu zaidi moyoni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni