B.B. King - ambaye anatambuliwa kuwa bingwa wa muziki aina ya Blues ulimwenguni amefariki akiwa na miaka 89.
Jinsi anavyocheza gita lake kuliathiri pakubwa kizazi cha wacheza gitaa.Alizaliwa Mississippi huko Marekani kulikokuwa na pamba na akafanya kazi katika mashamba akiwa bado mdogo.
Kisha aliajiriwa kama mwimbaji katika miaka ya arobaini kabla ya kuwa 'deejay' na baadaye kuanza muziki wake mwenyewe.
Alicheza katika hafla zilizovutia watu wengi akitumbuiza watu vizuri licha ya kuwa na umri wa miaka 80
Alisitisha ziara yake ya Marekani na Ulaya ili kuwatembelea wanawe 15 ambao aliwapata kupitia ndoa zake mbili zilizovunjika kutokana na umaarufu wake
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni