Ijumaa, 15 Mei 2015

Balaa la Wakimbizi wa Kiafrika Mediterania

Wakimbizi takriban 100 ambao walisema walikuwa baharini kwa siku 12 waliokolewa Jumatano wiki ya kwanza ya mwezi Mei mwaka 2015 na walinzi wa pwani wa Italia.
Umoja wa Mataifa Jumatatu (11.05.2015) uliarifiwa kuhusu janga la wahamiaji katika bahari ya Mediterenia na mapendekezo yatakayowalenga wafanyabisahara haramu ya kusafirisha binadamu wanaozidi kuuchochea mzozo huo.
Kuokolewa kwa watu hao, theluthi moja kati yao wakiwa wanawake, ambao watatu walikuwa wajawazito, ni tukio la hivi karibuni la kuokolewa maelfu ya wakimbizi wanaojaribu kuingia Ulaya kutumia boti za walanguzi. Wengi wao wamekuwa wakianzia safari yao kutoka pwani ya Libya, ambako wafanyabiashara ya kusafirisha binadamu wamekuwa wakiendesha shughuli zao bila hofu ya kukamatwa wala kuchukuliwa hatua yoyote kisheria na wakiutumia mzozo wa kisiasa na machafuko yanayoendelea nchini humo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni