Ijumaa, 15 Mei 2015

ABIRIA 12 WANUSURIKA KIFA HUKO PEMBA

 
 Ndege hiyo  ikiwa kwenye majani
Abiria 12 wamenusurika kufa baada ya ndege waliyokuwa wamepanda kukosea njia na kuingia kwenye nyasi wakati ikitua kwenye uwanja wa Karume mjini Chakechake Pemba. 


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa kusini Pemba kamishina msaidizi Juma Yusufu Ali ametaja ndege iliyokumbwa na tukio hilo kuwa ni AIR SALAMU N0 5H –HAD iliokuwa ikitokea Unguja. 


Amesema katika tukio hilo abiria mmoja Mohamed Zahoro Yahaya mwenye miaka 21 mkazi wa Kichungwani Chakechake amepata mshituko na amelazwa katika hospitali ya Chakechake. 


Dr. wa zamu wa Hospitali ya Chakechake Khamisi Masod amesema hali ya abiria huyo anaendelea na matibabu jamaa wa mjeruhiwa huyo Suleiman Yahaya Suleiman amesema hali ya ndugu yake inaendelea vizuri huku akiwa anaendelea na matibabu. 


ITV kisiwani Pemba imefika hadi uwanja wa ndege wa Karume kisiwani Pemba na kuonana na meneja wa uwanja huo hakuweza kusema chochote na kudai kuwa yeye si msemaji na baadae kupanda ngazi hadi kwa meneja wa mamlaka wa viwanja vya ndege Tanzania TCAA lakini naye akakata kutoa ushirikiano juu ya tukio hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni