Jumatano, 23 Aprili 2014

GABI ACHUKIZWA NA CHELSEA `KUPAKI BASI`, TERRY, CECH WAUMIA!!

389319_heroa
BAADA ya suluhu pacha ya bila kufungana ( 0-0) na Chelsea, nahodha wa Atletioc Madrid, Gabi amekerwa na mbinu ya `kupaki basi` waliyotumia wapinzani wao katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali, ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Atletico wanaosifiwa kujilinda katika ligi ya Hispania, La Liga wamekutana na timu ya Chelsea ambayo ina uwezo mkubwa wa `Kupaki basi` kwenye ligi ya England.
Katika nusu fainali hiyo ambayo haitasahaulika kwa Atletico, vinara hao wa La Liga walimiliki mpira kwa asilima 62 na kupiga mashuti 26 golini, wakati Chelsea walipiga mashuti matano tu.
Matokeo ya leo yanaonekana kuwa mazuri kuelekea mechi ya marudiano darajani Stamford, ambapo washambiliaji wawili wa Chelsea Eden Hazard na Samuel Eto`o watarejea uwanjani.
Gabi amekiri kuwa matokeo ya leo yamewaacha katika hatari kubwa.
“Hatujaridhika, lakini mechi bado. Atletico walihitaji kushinda kutoka mwanzo wa mchezo hadi mwisho”.
“ Tulijua Chelsea wasingekubali kufungwa kirahisi na mwisho wa siku tumetoka kapa”. Gabi amewaambia waandishi wa habari.
Atletico hawajafungwa katika michuano ya kimataifa mwaka huu, lakini matokeo ya leo yamewafanya washindwe kupata ushindi kwa mara ya kwanza katika michuano ya ulaya msimu huu wa 2013/2014.
Katika mechi ya jana usiku, Chelsea wamepatwa na majanga baada ya nahodha wake, John Terry na mlinda mlango namba moja, Petr Cech kupata majeraha.
 
Leo nusu fainali ya pili itashuhudiwa katika dimba la Santiago Bernabeu ambapo Real Madrid watawakaribisha mabingwa watetezi, Bayern Munich mechi ambayo ni kama fainali kutokana na timu zote  mbili kuwa ni timu kubwa na zenye wachezaji mahiri (TK).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni