Jumatatu, 22 Septemba 2014

LIVERPOOL HOI YACHAPWA 3-1 NA WESTHAM UNITED

Liverpool yaambulia kichapo cha 3 msimu huu dhidi ya West Ham
Liverpool iliambulia kichapo chake cha tatu katika mechi 5 za ligi kuu ya premia ya Uingereza huko Upton Park.
Washindi hao wa pili msimu uliyopita walitarajiwa kuwalaza West Ham lakini wenyeji hao hawakutaka kuwapisha.
Winston Reid alifungua kichapo hicho kwa bao la kwanza kunako dakika ya pili tu ya mechi hiyo kisha Diafro Sakho akafunga la pili katika dakika ya Saba .
Kuanzia hapo Vijana wa Brenda Rodgers hawakuwa na jibu dhidi ya Sam Allardyce hadi dakika ya 26 Raheem Sterling alipoifungia Liverpool bao la kufutia machozi.
Hata hivyo The Hammers hawakuwa wamekamilisha kivuno hicho kwani Morgan Amalfitano alimhakikishia Sam Allardyce alama tatu muhimu na ushindi wa kwanza kwa mashabiki wa Upton Park.
West Ham ilikuwa imeshindwa katika mechi zake za kwanza uwanjani Upton Park na mashabiki walitarajia kupoteza alama zingine.
Kipa wa West Ham Adrian aliibua hamaki za Mario Balotelli, na kupelekea muitaliano huyo machachari kupewa kadi ya njano.
Mechi hiyo ndiyo iliyokuwa ya mwisho kuchezwa Jumamosi
Mechi nyingine zilizochezwa siku ya jumapili ilikuwa ni kati ya Queen Park Rangers wakiwa nyumbani ambayo ilitoka sare ya 2 - 2 na Stoke City.
Mame Biram Diouf ndiye aliyekuwa wa kwanza kuandika goli kwa upande Stoke katika dakika ya 11 ambapo baadae katika dakika ya 42 Steven Caulker aliisawazishia QPR goli.
Peter Crouch aliongeza bao kwa upande Stoke katika 41 muda mfupi kabla ya mapumziko japo goli hilo halikudumu kwani katika dakika ya 88 Niko Kranjcar aliisawazishia QPR

Matokeo mengine ya mechi za Jumamosi
  • QPR 2 - 2 Stoke City
  • Aston Villa 0 - 3 Arsenal
  • Burnley 0 - 0 Sunderland
  • Newcastle 2 - 2 Hull City
  • Swansea 0 - 1 Southampton

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni