Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya mvua kubwa kunyesha tena kuanzia leo na kesho katika ukanda wa Pwani.
Katika taarifa yake kwa umma jana jioni, TMA
imesema maeneo ambayo yataathiriwa na mvua hizo za kuanzia leo ni Visiwa vya
Unguja na Pemba pamoja na mikoa ya Tanga, Pwani na Dar es
Salaam.
Huo ni mwendelezo wa mvua zilizosababisha
maafa makubwa ambazo zilianza kunyesha Aprili 10, mwaka huu katika ukanda huo wa
pwani. Maeneo yaliyokuwa yameathiriwa zaidi ni Dar es Salaam na Morogoro ambako
zaidi ya watu 25 walifariki dunia.
Mbali ya vifo hivyo, mvua hizo zilisababisha
uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara hasa madaraja.
Mawasiliano ya barabara kati ya Mkoa wa Dar
es Salaam na mingine nchini yalikatika kwa siku mbili baada ya barabara zake
zote zinazouunganisha na maeneo hayo ama kuharibiwa vibaya na mafuriko au kujaa
maji na kushindwa kupitika.
Taarifa hiyo ya TMA imesema mvua hizo
zinatarajiwa kuwa kubwa kwani zitazidi milimita 50 katika saa
24.
“Wakazi wa maeneo ya hatari, watumiaji wa
bahari pamoja na mamlaka zinazohusika na maafa, wanashauriwa kuchukua tahadhari
stahiki,” ilisema taarifa hiyo.MWANANCHI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni