Ijumaa, 22 Agosti 2014

BASI LAPIGWA BOMU KIGOMA WATATU WAFARIKI

Picha ya maktaba bomu likiwa limetegwa ardhini.

KIGOMA. Watu watatu wamekufa akiwepo mtoto mchanga na wengine sita kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria (Hiace) kurushiwa bomu na watu wasiojulikana huko Kasesema, Kigoma alfajiri ya leo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Buhigwe (OCD), Samwel Utonga alisema basi hilo lilikuwa likotokea Kilelema kwenda Kasulu Mjini ambapo watu hao walisimamisha basi hilo kwa nia ya kuwapora abiria lakini dereva akawa jasiri na kuwapita ndipo walipolirushia kitu kinachoaminika kuwa ni bomu.


Taarifa kutoka Hospitali ya Muyama zinazema majeruhi hao wamehamishwa toka hospitalini hapo na kupelekwa Hospitali ya Kasulu baada ya hali zao kuwa mbaya.Chanzo MWANANCHI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni