Kitengo cha sheria nchini ya Marekani kimeanza kufanya
uchunguzi wa jinai dhidi ya kifo chamwandishi wa habari mwenye asili ya Marekani , James Foley aliyeuawa na wapiganaji wa kiislamu wenye msimamo mkali.
Mwanasheria mkuu wa kitengo hicho, Eric Holder ameweka wazi kuwa wote
waliohusika na mauaji ya mwandishi huo watawatia mkononi muda si mrefu.
Maofisa wa serikali ya Marekani wandai kwamba askari hao wauaji walidai kiasi
kikubwa cha pesa zipatazo dola za kimarekani zaidi ya milioni mia moja na
thelathini kama fidia ya kumuachilia James Foley.
Marekani imekwisha anza harakati za kuwasaka na hatimaye kuwakamata
waliohusika na mauaji ya mwandishi huyo kwa kurusha ndege zake takriban sita
katika anga inayomilikiwa na waislamu kaskazini mwa Iraq.
Pamoja na kwamba waislam hao kutishia kumuua mmarekani mwingine
wanayemshikilia kama ulipizaji wa kisasi endapo mashambulio yataelemea upande
wao bado Marekani imesisitiza kuwakamata wahusika (BBC)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni