Timu ya Manchester United ya England imekutana na kipigo cha mbwa mwizi baada ya kuongoza kwa mabao 2 - 1 katika kipindi cha kwanza. Kikosi cha Man U kilikuwa kiekamilika kama inavyoonekana hapa chini
Mchezaji wa Man U di Maria akiwatoka walinzi wa Leicester City
Man U ndio waliokuwa wa kwanza kufunga bao baada ya Facao kumpa mpira van Persie ambaye alifunga bao katika dakika ya 13. Katika dakika ya 16 di Maria aliwanyanyua mashabiki wa Man U baada ya kuifungia bao la pili.
Leicester City waijitutumua na kufunga goli lake la kwanza katika dakika ya 17 kupitia kwa Ulloa. Hadi mapumziko Man U 2 Leicester City 1.
Kipindi cha pili Man U waliongeza bao la tatu katika dakika ya 57 mfungaji akiwa ni Herrera. Baada ya hapo Leicester City walichachamaa na kufunga mabao manne - Nugant alifunga bao kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 62 na Cambianso akaweka bao la kusawazisha katika dakika ya 64.
Katika dakika ya 79 Vardy akaifungia Leicester bao la nne na katika dakika ya 83 Ulloa akahitimisha karamu ya magoli kwa penalti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni