WATU 4 WAFARIKI DUNIA JIJINI NAIROBI BAADA YA NDEGE YAO KUANGUKA
Shughuli za uokoaji zikiendelea baada ya ndege ya mizigo
kuanguka jijini Nairobi
Watu wanne akiwemo Rubani wa ndege moja ya mizigo, wamefariki
dunia baada ya ndege walimokuwa kuanguka mapema leo asubuhi katika mtaa wa
Embakasi jijini Nairobi.
Kwa mjibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya, ndege hiyo ilianguka
dakika chache tu baada ya kuruka kutoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Jomo Kenyatta.
Ndege hiyo ya mizigo ilikuwa imebeba shehena ya Miraa ama Mairungi kuelekea
Mogadishu nchini Somalia.
Uchunguzi umeonyesha kuwa ndege hiyo huenda iligonga mlingoti wa umeme karibu
na mtaa wa Embakasi, mjini Nairobi na kuanguka
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni