Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimkaribisha ofisini kwake
Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad (kushoto) kwa ajili ya
kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya
Norway na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri
huyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Balozi Simba Yahya. Picha na zote Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa
Japan nchini, Ian Myles (wapili kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea
ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana masuala
mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japan. Wapili kushoto ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara hiyo, Haji Janabi, na
kulia ni Msaidizi wa Balozi huyo, Pascale Julien. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa
Norway hapa nchini, Hanne-Marie Kaarstad (kulia) wakati Balozi huyo
alipomtembelea Waziri Nchemba ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo
kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania
na Norway. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsikiliza Balozi wa India
hapa nchini, Sandeep Arya (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea
Waziri huyo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya
kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa
Rwanda, Eugene Kayihura (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri
Nchemba ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili
masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akipokea zawadi kutoka kwa
Balozi wa India nchini, Sandeep Arya (kulia) mara baada ya Balozi huyo
kumaliza mazungumzo na Waziri ambayo yalifanyika ofisini kwake, jijini
Dar es Salaam leo. Mazungumzo hayo yalikuwa na lengo la kujadili masuala
mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsindikiza Balozi wa Rwanda,
Eugene Kayihura (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao,
yaliyofanyika ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Lengo
la mazungumzo hayo ni kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya
nchi jirani ya Rwanda na Tanzania. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni