MKURUGENZI wa Mashitaka
Nchini (DPP), amemfutia mashitaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,
Gabriel Fuime (61) na kisha kumuunganisha na wenzake 11 na kuwasomea upya
mashtaka 27 ya mauji katika mtaa wa Indira Gandh, yaliyotokana na kuporomoka
jengo la ghorofa 16.
Mbali na Fuime washtakiwa
wengine ni, Diwani wa Kata ya Goba, Ibrahim Mohamed maarufu kama Kisoki, Raza
Ladha, Goodluck Mbanga, Willbroad Mugyabuso,Mohamed Abdulkarim, Charles Ogare,
Zonazea Oushoudada, Vedasto Ruhale, Michael Hema, Albert Mnuo na Joseph
Ringo.
Washtakiwa hao walisomewa
hati mpya ya mashitaka baada ya kuondolewa hati ya zamani ya mauaji ya bila
kukusudiwa na kuunganishwa Fuime na idadi yao kufikia 12, mbele ya Hakimu Mkazi
Devota Kisoka.
Upande wa Jamhuri
uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Benard Kongola akisaidiana na Wakili wa
Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka na Wakili wa Serikali Joseph
Maugo.
Kongola alidai kuwa kwa
mujibu wa kifungu kidogo cha 294 kidogo cha (1) upande wa Jamhuri unaomba ridhaa
ya mahakama ya kumuongeza mshtakiwa Fuime katika hati mpya ya
mashitaka.
Hakimu Kisoka alisema
mahakama haina pingamizi na maombi ya Jamhuri ya kubadilisha hati ya mashitaka
dhidi ya washtakiwa.
Jamhuri ilidai kuwa katika
shitaka la kwanza, Machi 29, mwaka 2013 mtaa wa Indira Gandh, Wilaya ya Ilala
washtakiwa kwa pamoja walimuua kwa makusudi Yusuph Khari.
Alidai katika shitaka la
pili na la tatu, Machi 29, mwaka 2013 washtakiwa waliwaua kwa makusudi Kulwa
Alfani na Hamada Musa.
Katika shitaka la nne na la
tano, ilidaiwa kuwa Machi 29, mwaka 2013 katika mtaa huo, washtakiwa wote kwa
pamoja waliwaua kwa makusudi Kessy Manjapa na Khamis
Mkomwa.
Kongola alidai katika
shitaka la sita na la saba, Machi 29, mwaka 2013 katika mtaa huo, washtakiwa
waliwaua kwa makusudi Boniface Bernard na Suhail Karim.
Upande huo wa Jamhuri
ulidai katika shitaka la nane na la tisa, Machi 29, mwaka 2013 katika mtaa huo,
washtakiwa wote kwa pamoja waliwaua kwa makusudi Salmani Akbar na Selemani
Haji.
Wakili wa serikali Maugo
aliendelea kusoma hati hiyo ya mashtaka alidai katika shtaka la 10 na 11, Machi
29, mwaka 2013 katika mtaa huo, washtakiwa wote kwa pamoja waliwaua kwa makusudi
Selemani Mtego na Sikudhani Mohamed.
Ilidaiwa katika shitaka la
12 na 13, Machi 29, mwaka 2013 katika mtaa huo, washtakiwa wote kwa pamoja
waliwaua kwa makusudi Ahmed Milambo na Salum Mapunda.
Shtaka la 14 na 15,
ilidaiwa kuwa Machi 29, mwaka 2013 katika mtaa huo, washtakiwa wote kwa pamoja
waliwaua kwa makusudi Suleimani Mnyani na John Majewa.
Shtaka la 16 na 17,
ilidaiwa kuwa Machi 29, mwaka 2013 katika mtaa huo, washtakiwa wote kwa pamoja
waliwaua kwa makusudi Mussa Mnyamani na David Herman.
Maugo alidai katika shitaka
la 18 na la 19 kwamba Machi 29, mwaka 2013 katika mtaa huo washtakiwa waliwaua
kwa makusudi William Joakim na Abdulrahman Mwiha.
Alidai katika shitaka la 20
na 21 kwamba Machi 29, mwaka 2013 mtaa wa huo, washtakiwa wote kwa pamoja
waliwaua kwa makusudi Jumanne Athuman
na Advai
Mpinge.
Wakili huyo aliendelea
kusoma hati hiyo, shitaka la 22 na la 23, alidai kuwa Machi 29, mwaka 2013 mtaa
huo washtakiwa wote kwa mapoja waliwaua kwa makusudi Emmanuel Wahai na Agustino
Chuma.
Katika shitaka la 24 na 25,
ilidai kuwa Machi 29, mwaka 2013 katika mtaa huo, washtakiwa wote kwa pamoja
waliwaua kwa makusudi Phillipo Kusimala na Said Abbas.
Maugo aliendelea kudai
katika shitaka la 26 na 27, Machi 29, mwaka 2013 katika mtaa huo, washtakiwa
wote kwa pamoja waliwaua kwa makusudi Bethod Mwanengule na Gabriel Kamwela
.
Kwa mujibu wa Mwenendo wa
Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA), mashitaka yanayowakabili washtakiwa hawatakiwi
kujibu chochote hadi pale upelelezi wa kesi hiyo utakapokamilika itahamishiwa
Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kwa ajili ya
kusikilizwa.
Hakimu Kisoka alisema kesi
hiyo itatajwa Machi 26, mwaka huu na washtakiwa dhamana yao imefutwa wapelekwe
mahabusu.
Jana saa 3:00 asubuhi
upande wa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Augustino Mmbando uliwasilisha hati ya
Nole kutoka kwa DPP ikieleza kwamba hana nia ya kuendelea kumshitakiwa Fuime na
kuomba kumfutia mashtaka hayo.
Hakimu Mmbando alifuta
mashitaka hayo, lakini askari kanzu wa jeshi la Polisi walimuweka chini ya
ulinzi na baadaye alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Kisoka na kuunganishwa
na wenzake
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni