Jumamosi, 22 Februari 2014

UGANDA: MSWADA DHIDI YA PICHA ZA NGONO WATIWA SAINI


Rais Yoweri Museveni wa Uganda atia saini mswada wa sheria dhidi ya picha za ngono.
Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda atia saini muswada wa sheria dhidi ya picha za ngono.
Ikiwa unaishi Uganda na unapenda kuvaa nguo fupi, zinazobana  au zinazoonyesha sehemu za mwili ambazo zaweza kuwafanya watu wa jinsi nyingine kusisimkwa na kutamani kushiriki ngono nawe, basi jua uko taabuni.

Hii ni kwa sababu rais Yoweri Museveni ametia saini mswada dhidi ya picha za ngono ambao unapinga mavazi yasiyo ya heshima haswa yanayovaliwa na wanamuziki na picha za watu wakiwa uchi. (TK)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni