Jumatano, 12 Machi 2014

MABAKI YANAYOFANA NA YA NDEGE YAONEKANA BAHARINI


Picha zilizonaswa na mtambo wa satellite
Serikali ya Uchina imechapisha picha zilizonaswa na mtambo wake wa satelite zikionesha mabaki ya kitu kipana kikielea katika bahari ya Kusini mwa Uchina. Picha hizo zilipigwa siku ya Jumapili, saa ishirini na nne baada ya ndege ya abiria ya Malaysia kutoweka ikiwa na abiria 239, lakini haijabainika ikiwa vifaa hivyo ni vya ndege hiyo. Huku ikiwa na raia wake 154, ambao walikuwa abiria kwenye ndege hiyo ya Malaysia, serikali ya Uchina imetuma mitambo kumi ya satellite kusaidia katika harakati za kutafuta ndege hiyo. Picha za vifaa hivyo vitatu, ambavyo moja ina upana wa takriban mita 24 kwa 22, zilichukuliwa siku ya Jumapili, siku moja tu baada ya ndege hiyo kupotea, lakini zilichapishwa siku ya Jumatano.


Picha zilizonaswa na mtambo wa satellite

Ubawa wa ndege hiyo iliyopotea ina upana wa mita sitini na moja.
Picha hizo za satellite zimeweka vifaa hivyo takriban maili mia moja kutoka kwa njia iliyotarajiwa kutumiwa na ndege hiyo na sio mbali kutoka katika kisima kimoja cha mafuta, ambako mfanyakazi mmoja aliripoti kuona kitu kilichokuwa kikichomeka angani siku ya Jumamosi asubuhi.
Lakini siku chache zilizopita, kumekuwa na fununu kadhaa kuhusiana hatma ya ndege hiyo lakini zote zimekuwa za uongo.
Makundi ya uokozi  vile vile wanatafuta mabaki ya ndege hiyo katika maji karibu na rasi ya Malaysia, kwa sababu wanaamini kuwa ndege hiyo ya Malaysia ilibadili mkondo na kuelekea Magharibi.


Picha zilizonaswa na mtambo wa satellite
NA BBC SWAHILI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni