WAHOFIWA KUFA KWA MAFURIKO NCHINI INDIA
Watu kadhaa wanahofiwa kufa baada ya basi walilokuwa
wakisafiria kuchukuliwa na maji katika jimbo la Kashmir nchini India. Basi hilo
lilikuwa limebeba abiria hamsini waliokuwa wanatoka katika sherehe za harusi akiwemo bibi
na bwana harusi.
Afisa wa polisi katika eneo la Kashmir Owais Ahmad ameiambia BBC kuwa
mafuriko yanazidi kuongezeka na jitihada za uokoaji zinaendelea.
Eneo hilo
limekumbwa na mafuriko makubwa kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 22,
ambapo watu tisa wamepoteza maisha tangu mafuriko hayo yaanze Jumanne wiki hii (TK).
Ajali
za barabarani nchini India zimekuwa zikitokea mara kwa mara ambapo takwimu za
serikali zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 138,000 walikufa mwaka jana, 2013
kutokana na ajali hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni