Jumamosi, 12 Desemba 2015

MSAADA MKUBWA UNAHITAJIKA KWA DADA ELIZA ILI AWEZE KUFANYIWA UPASUAJI WA UVIMBE TUMBONI


 
Eliza Juma (30), mkazi wa Mtaa wa Mbwanga Manispaa ya
Dodoma anaomba msaada wa hali na mali kutoka kwa yeyote ataeguswa ili aweze
kufanyiwa upasuaji wa uvimbe tumboni ambao umekuwa ukiongezeka kila siku.
Akizunguma na waandishi wa habari mjini hapa Dodoma, alisema kuwa
uvimbe huo ambao umekuwa ukiongezeka kila siku umekuwa kikwazo kwake katika
kutekeleza majukumu yake ya kujipatia kipato.
Alisema kuwa uvumbe huo unaotokana na yeye kufanyiwa upasuaji wa utumbo aliofanyiwa miaka miwili iliyopita kutokana na utumbo wake kujikunja.
“Nilifanyiwa upasuaji wa utumbo miaka miwili iliyopita katika hospitali ya mkoa wa Dodoma ambapo utumbo wangu ulikuwa umejikunja lakini mara baada ya kufanyiwa upasuaji huo kidonda kilianza kuwasha na mimi nikawa napakuna ndipo pakaanza kuvimba hadi kufikia ukubwa huu unaouona sasa” alisema Eliza.
Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo alikwenda hopitali ya mkoa ili kuweza kuonana na daktali ambaye alimweleza kuwa tatizo hilo linatokana na ngozi ya ndani kulika hivyo anatakiwa kufanyiwa upasuaji kwa
mara nyingine.
Aidha alisema kuwa kutokana na hali yake ya kiuchumi na kiasi alicho ambiwa kulipia ili aweze kufanyiwa upasuaji huo yeye hawezi kumudu
kwa kuwa hana msaada wowote anaoutegemea zaidi ya wasamairia wema.
“Kiasi kinachohitajika ili niweze kufanyiwa upasuaji ni zaidi ya shilingi laki tatu na mie kama mnavyoniona hapa nilipo natunzwa na wasamiria wema sina mama wala baba hivyo nawaomba wasamaria wema kunisadia ili niweze kupata kiasi hicho kwa ajili ya matibabu kabla tatizo halijawa kubwa
zaidi”alisema Eliza.
Alisema kuwa kwa yeyote atakayeguswa anaweza kumchangia anaweza kuwasiliana naye kupitia namba ya simu ya mkononi 0678164633
ili aweze kupata kiasi hicho cha pesa na kupatiwa matibabu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni