Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba Dickson, akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ufugaji wa sungura unaweza
ukawasaidia wakulima katika kujiongezea kipato kwa mbali na kuuza nyama
yake lakini pia wana uwezo wa kuuza kinyesi, mkojo pamoja na ngozi
yake,katika ziara ya mafunzo kuhusu mradi huo katika eneo la Kivungwi
kata ya Vigwaza, Mkoa wa Pwani.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba Dickson,akiwaonesha waandishi
moja ya sungura wanaopatikana katika shamba hilo, kulia ni Mjasiriamali
na mfugaji wa sungura hao, Gladness Nyange, katika ziara ya mafunzo
kuhusu mradi huo katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoa wa Pwani.
Sehemu ya mabanda ya kufugia Sungura hao.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba akifafanua jambo kwa Wandishi
wa habari katika ziara ya mafunzo kuhusu mradi huo katika eneo la
Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoa wa Pwani.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii
WATANZANIA
wameshauriwa kujihusisha na ufugaji wa sungura ili waweze kujiongezea
kipato kutokana na mnyama huyo kuwa na faida nyingi.
Ushauri
huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba
Dickson wakati akizungumza na waandishi wa habari waliokuwa katika ziara
ya mafunzo kuhusu mradi huo jana katika eneo la Kivungwi kata ya
Vigwaza, Mkoani Pwani.
Dickson
alisema, ufugaji wa sungura unaweza utawanufaisha wakulima katika
kujiongezea kipato mbali na kuuza nyama yake wana uwezo wa kuuza
kinyesi, mkojo pamoja na ngozi yake
“Tunawafundisha
wakulima jinsi ya kufuga sungura ili waweze kunufaika, lakini wanaweza
kujiuliza ni wapi wanaweza kuwauza wakishafikia hatua ya kuuzwa, sisi
tunawapa soko kwa hiyo kikubwa kwa mkulima ni kufuga tu,” Dickson
alisema.
Alisema
kampuni yake ina mashamba ya sungura hivyo wanapoingia mkataba na
wakulima wanaohitaji kufuga wanakubaliana mambo mbalimbali ikiwemo
kuwatafutia masoko ambapo wao wenyewe wananunua sungura hao.
Alisema
mbali na faida ya kuuza nyama yake lakini pia wanaweza kuuza kinyesi,
mkojo pamoja na ngozi yake.
Naye
Mjasiriamali na mfugaji wa sungura hao, Gladness Nyange alisema, kuna
umuhimu wa kinamama kutumia fursa ya ufugaji sungura ili kumudu
kuwasomesha watoto wao badala ya kuwategemea waume zao.
Alisema
licha ya kuwa sungura hao wanahitaji uangalizi wa hali ya juu katika
kuwafuga lakini amekuwa akihakikisha kuwa wanaishi katika mazingira mazuri
ili waweze kumpa faida.
“Huu
ufugaji kwa kuwa ni mpya watu, wengi wanaweza kujiuliza inakuwaje au
masoko watapata wapi...lakini mimi nilipoanza kufuga niliingia mkataba
na hii kampuni na wao walinipa masoko ina maana kwa kila sungura wa kilo
nne nauza kwa Sh 40,000,” Nyange alisema.
Nyange
alishauri wajasiriamali na hasa wanawake kujiingiza katika ufugaji huo
ili waweze kufanya mambo yao mbalimbali bila kuwategemea akinababa ambao
wakati mwingine wanakuwa na majukumu memgi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni