Ashraf Ghani ameapishwa kuwa rais mpya wa Afghanistan, akichukua nafasi ya Hamid Karzai katika sherehe zilizofanyika ikulu ya rais mjini Kabul.
Kuapishwa kwa Bwana Ghani kunakuja baada ya miezi sita, huku kukiwa na mvutano mkubwa kuhusu kulalamikia udanganyifu katika kupiga na kuhesabu kura.Kwa mujibu wa mkataba uliosimamiwa na Marekani Bwana Ghani atashirikiana madaraka na mshindi wa pili katika uchaguzi wa urais Bwana Abdullah Abdullah ambaye atakuwa afisa mtendaji mkuu.
Kundi la Taliban limeupuuza mkataba huo kwa kuuita "igizo la Marekani". Mlipuko karibu na uwanja wa ndege wa Kabul umeua watu wapatao saba.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Sediq Sediqi amesema mtu aliyajilipua alishambulia kituo cha usalama cha ukaguzi katika barabara ya uwanja wa ndege inayoenda ubalozi wa Marekani.
Askari wanne wa usalama wa Afghanistan na raia watatu wameuawa na watu kadhaa kujeruhiwa, amesema.
Mabadiliko ya Kikatiba
Bwana Ghani ameapa kutii katiba katika sherehe za kuapishwa zilizohudhuriwa na viongozi 100.Amesema atafanya kazi ya mpango wa amani ya muda mrefu, ameahidi kupambana na rushwa na kusema kuwa mabadiliko ya katiba yanahitajika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni