Wizara ya Afya nchini Afrika Kusini inasema kuwa wavulana kumi
na tisa wameaga dunia mwaka huu katika sherehe za kitamaduni za kuwaingiza tohara
wavulana.
Tohara ndio utamaduni unaopewa heshima kubwa katika baadhi ya maeneo ya
taifa hilo.Vijana 19 wamefariki kufika sasa na wengine 50 wako hospitalini.
Wanapokea matibabu ya kukosa maji mwilini, sehemu zao za siri kuoza na majeraha mengine mabaya.
Wazee wa kijamii wasiokuwa na mafunzo ya kufanya tohara ambao huendesha vituo vya kuwaingiza tohara vijana wamelaumiwa kwa vifo kama hivyo.
Katika baadhi ya visa ambavyo vimeripotiwa, vijana hutoroka na kujiunga na vijana wengine wanaokwenda katika vituo hivyo haramu bila ya idhini ya wazazi.
Serikali imewasihi wazee wa kijamii kushirikiana na watu wenye uwezo wa kitaalamu na madaktari ili kuwapa tohara vijana na kuzuia vifo.
Mwezi jana watu 23 walikamatwa kwa vifo vya vijana waliofariki kutokana na athari za kupatia tohara
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni