Jumatatu, 24 Machi 2014

TRAFIK AGONGWA NA GARI MOROGORO.


Picha ya akari wa Usalama barabarani akisaidiwa na raia mwema baada ya kupata ajali
 
Askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Morogoro ambaye anajulikana kama Crispin 'Mandela' amegongwa na gari eneo la Mtawala Barabara inayotoka Msamvu kuingia katikati ya Mji wa Morogoro. Hii ni Mara ya tatu kwa Askari Huyo Kugongwa na Gari Mkoani Hapa.

Tukio hilo lilitokea jana wakati Askari huyo alipokuwa Eneo la Kituo cha kushusha Abiria Kwenye Shule ya Msingi ya Mtawala Mkoani hapa.
 
Kwa sasa Afande huyo amelazwa wodi namba moja hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro  na hali yake inaendelea vizuri (TK).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni