Alhamisi, 3 Julai 2014

AL SHABAB WAUA MBUNGE MAARUFU


Wanamgambo wa al-shabaab wa Somalia
Wanamgambo wa Al Shabab wamedai kuwa wamemuua kwa kumfyatulia risasi mbunge maarufu mjini Mogadishu.
Ahmed Mohamud Hayd aliuawa baada ya kutoka hotelini ambapo katika tukio hilo, mlinzi wake pia aliuawa na katibu wa Bunge alijeruhiwa mashuhuda wameeleza.
 
Kundi la Al-Shabab, ambalo lina uhusiano na al-Qaeda, limeapa kuendelea na mashambulizi zaidi katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Wanamgambo hao walipoteza ngome yao mjini Mogadishu na kuchukuliwa na Vikosi vya Umoja wa Afrika mwaka 2011 lakini wameendelea kutekeleza mashambulizi ya mabomu na mauaji mjini humo.
Msemaji wa kundi hilo Abdulaziz Abu Musab amesema kuwa kundi lake limetekeleza mauaji kama ilivyopangwa na kuwa wataendelea kuwafuatilia Wabunge wengine ikiwa hawataachana na Bunge.
Al-Shabab imekuwa ikipigania kuunda taifa la kiislamu nchini Somalia

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni