Tetemeko la ardhi la nguvu ya
5.7 katika vipimo vya Richter lilitokea eneo la Bukoba, kaskazini
magharibi mwa Tanzania Jumamosi na kusababisha maafa.
-
Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa takriban kilomita 44 kutoka mji wa Bukoba, ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Kagera, kwa mujibu wa taasisi ya jiolojia ya Marekani.
-
Watu 16 wamethibitishwa kufariki na wengine 180 kujeruhiwa.
-
-
Nyumba nyingi ziliporomoka na kuwaacha mamia ya watu wakiwa bila makao.
-
Tetemeko hilo ndilo mbaya zaidi kukumba Tanzania katika kipindi cha zaidi ya mwongo mmoja. Mitetemeko ilisikika maeneo ya Uganda, Kenya, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.-
Rais wa Tanzania John Magufuli ameahirisha ziara ya siku tatu ambayo alitarajiwa kuifanya nchini Zambia.
-
Miongoni mwa mengine, Dkt Magufuli angehudhuria kuapishwa kwa Rais Edgar Lungu lakini sasa atawakilishwa na makamu wake Bi Samia Suluhu Hassan.-
Bw Zaka Khamis, mmoja wa wakazi wa Bukoba, ni miongoni mwa waathiriwa.
-
Nyumba yake iliporomoka kutokana na tetemeko hilo la ardhi lililotokea mwendo wa saa tisa unusu alasiri.-
- Waathiriwa wanaomba msaada kuwasaidia kurejelea katika hali yao ya kawaida.
-
- Picha hii ya filamu ya Titanic, inayoangazia kuzama kwa meli ya Titanic, inaonekana miongoni mwa vifusi.
-
-
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amempigia simu Dkt Magufuli kumpa pole pamoja na watu wa Tanzania. Ameahidi kwamba jeshi la Kenya litatuma msaada wa mabati, blanketi na magodoro. Jumanne.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni