Alhamisi, 27 Oktoba 2016

WAZIRI MAKAMBA AKAMILISHA ZIARA KATIKA MKOA WA KATAVI

 Bibi Josephine Rupia, Mkuu wa Idara ya Maliasili Halmashauri ya Mpanda akitoa maelezo ya Mto Katuma kupoteza mwelekeo wa kutiririsha maji katika mkondo wake kama ilivyokuwa hapo awali.
Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akihutubia wananchi wa kijiji cha Kabage kilichopo Mkoani Katavi na kuwasisitizia umuhimu wa Hifadhi ya Mazingira
Mmiliki wa Kiwanda cha kutengeneza chumvi cha Nyanza Mining akitoa maelezo kwa Waziri Makamba juu uzalishaji wa chumvi hiyo kwa kutumia nishati ya jua.


TAARIFA YA ZIARA YA MHE. JANUARY MAKAMBA KATIKA MKOA WA KATAVI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na  Mazingira  Mhe January Makamba hii leo ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Katavi kwa kutembelea kijiji cha Kabege ambapo aliangalia mradi Mkubwa wa Umwagiliaji wa Mwamkulu katika Manispaa ya Mpanda ambao kwa sasa umesitisha kutoa huduma zake kwa kukosekana kwa maji ya kutosha katika Mto Katuma.

Katika kikao cha Majumuisho ya Ziara yake ya siku mbili katika Mkoa wa Katavi, Waziri Makamba ameutaka uongozi wa Mkoa huo kudhibiti yafuatayo:
1.    Ongezeko la watu na mifugo ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia uharibifu wa mazingira. 
2.    Kusitisha uchepushaji kwa Mto Katuma ambapo taarifa ya Mkoa ilieleza kuna jumla ya mabanio 40 ambayo yanatumiwa na watu kuchepusha maji kwa ajili ya manufaa yao binafsi.
3.    Uchimbaji hatari wa Madini usiofuata taratibu
4.    Kuhuisha sheria ndogo ndogo za mazingira katika ngazi mbalimbali za Serikali za mitaa
5.    Kuanisha maeneo maalumu ambayo yatatangazwa katika Gazeti la Serikali kama mazingira nyeti ili kuyapa ulinzi zaidi
6.    Kusimamia uondoshwaji wa wavamizi katika Vyanzo vya maji 
7.    Kufanyika kwa sensa ya mifugo ili kujua Mkoa una mifugo kiasi gani na kubuni namna bora ya kuhumudimia mifugo hiyo bila kuathiri mazingira 
8.    ameahidi kuaanda andiko maalumu la Mradi wa Ziwa Katuma
9.    Mmiliki wa Jema Sitalike Project kutafutwa popote alipo, leseni yake ya madini isitishwe, apigwe faini na kurekebisha eneo alilokuwa akitumia awali kwa shughuli za uchenjuaji wa dhahabu.
10.  Waziri Makamba meagiza Watendaji kata na Vijiji kutotoa vibali vya uchimbaji wa madini bila kufuata utaratimu wa Wizara ya Nishati na Madini

Mara baada ya Majumuisho Waziri Makamba alipata fursa ya kuongea na wanakijiji cha Kabage na kusisitiza yafutayo:
1.    Wananchi kutunza mazingira kwa kutofanya kilimo cha kuhamahama, Ukataji Ovyo wa Miti na Uchomaji wa misitu.
2.    kuwakumbusha wananchi kuwa rasilimali ya maji ni ya watu wote hivyo isiwanufaishe watu wachache
3.    Serikali inaangalia namna bora ya kurudisha Mto Katuma katika njia yake ya awali ambayo ilipotea baada ya kutokea kwa mafuriko mwaka 1998
4.    Kuundwa kwa jumuiya za watumia maji na kuzingatia Sheria ya Mazingira ya kutofanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya mita sitini za chanzo cha maji
5.    Kuundwa kwa Kamati ya Mazingira katika Kijiji hicho
6.    Kuondokana na Makazi holela kwa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Waziri Makamba amewasili Katika Mkoa wa Kigoma na kutembelea kiwanda cha Nyanza Mines na kuwapongeza kwa kuzalisha chumvi kwa kutumia nishati ya jua ambapo awali kiwanda hicho kilifungiwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutokana na uharibifu wa Mazingira kwa kutumia magogo mengi mwaka 2015. Kiwanda hicho kwa sasa kinazalisha tani 20,000-25,000 ndani ya miezi mitatu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni