Alhamisi, 3 Julai 2014

POLISI WAUA MAJAMBAZI 5 KENYA

Nairobi, Kenya: Watu 5 wanaoshukiwa kuwa ni majambazi wameuawa katika matukio mawili tofauti leo nchini Kenya. Bastola 2 zilikamatwa baada ya majambazi kumpiga risasi na kumjeruhi mfanyabiashara mmoja jijini Nairobi.

Wanne kati yao walimpiga risasi na kumjeruhi mfanyabiashara mmoja jijini Nairobi na kujaribu kumpora sh za Kenya 200,000 (sawa na sh milioni nne za Kitanzania) alizokuwa amebeba kutoka katika supermarket katika Syokimau Railway station kabla ya kuuliwa na polisi.

Moja ya bastola zilizokamatwa iligundulika kuwa ni ya polisi na haijulikani ilwafiaje majambazi na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Walimpiga risasi mfanyabiashara huyo wakati akiingia kwenye gari lake na kuanza kumpora fedha hizo lakini mlio wa risasi uliwashtua polisi waliokuwa doria karibu na eneo hilo.

Mashuhuda wa tukio hilo pamoja na polisi walisema polisi waliwafukuza majambazi hao ambapo walifanikiwa kuwaua majira ya saa 6:30

Msaidizi wa mkuu wa polisi jijini Nairobi Moses Ombati alisema mshukiwa wa tano alifanikiwa kutoroka baada ya kutupa pikipiki mbili walizokuwa wakitumia. Mtuhumiwa mwingine aliuawa katika tukio jingine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni