Alhamisi, 3 Julai 2014

TANZANIA YANUFAIKA NA MRADI WA BIOGAS

Biogas inaendeleaa kuwa chanzo muhimu cha nishati ya kupikia nchini Tanzania. Inapunguza utegemezi wa aina nyingine za nishati mfano mafuta ya taa jambo ambalo linatufanya tufikirie upya juu ya majukumu ya jinsia mbalimbali.
A farmer feeding a cow
Diana Mangula anasema kuwa kupika kumekuwa rahisi kuliko alipokuwa anatumia kuni.

Mangula hakuwa anafurahia upishi wa kutumia kuni kwani ulikuwa unajaza moshiu kwenye jiko lote na kuta zake kuwa nyeusi.. Lakini kama walivyo wakazi wengi wa kijiji cha Ibumila katika mkoa wa  Njombenchini Tanzania, sasa amegundua kuwa nishati ya kinyesi cha ng'ombe ni safi na inasadia sana katika kupiga na pia kuwashia taa,

Diana Mangula cutting grass for her cowsDiana Mangula akikata majani kulishia ng'ombe
Kufuatia taarifa za watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mjini Morogoro, biogas inazidi kupata ummarufu Mkoani Njombe,

Mradi wa pamoja kati ya  Norwegian University of Life Sciences (NMBU) na  SUA unaangalia uzalishaji wa ng'ombe mkoani Njombe.

A female farmer proudly holds a bunch of carrotsMabaki yanayotokana na kinyesi cha ng'ombe ni mbolea nzuri
 
Programu ya Tanzanian Domestic Biogas  (TDBP), ambayo inasimamia mradi huo inasema kuwa biogas imerahisisha maisha ya watu wa vijijini.
Mradi wa Miaka mitano
A woman mixes cow dung and water while a man watchesKinyesi cha ng'ombe kikichanganywa na maji kabla ya kuanza kukitumia.
 
Biogas ilianza kutumika mkoani Njombe mwaka 2004 kwa nia ya kutoa nishati salama ya kupikia.na rafiki wa mazingira. Chini ya Mtadi huu wa  "Enhancing Pro-Poor Innovations in Natural Resources and Agricultural Value Chains" (EPINAV). unaofadhiliwa na serkali ya Norwey, wakulima wanajifunza namna bora ya kuboresha kilimo.
Profesa Ndelilio Uriyo, ambaye pia ni mtalam wa kilimo hifadhi amesema kuwa mabaki ya kinyesi ni mbolea bora sana

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni