Taarifa kutoka Kaskazini Mashariki mwa Nigeria zinasema kuwa
zaidi ya wanawake 60 wakiwemo wasichana wa umri mdogo waliotekwa nyara mwezi
jana na Boko Haram wametoroka.
Taarifa hii inakuja sawa na taarifa za kutokea makapigano makali kati
ya jeshi la Nigeria na wapiganaji wa kundi hilo.Serikali ya Nigeria imeitisha uchunguzi wa kina juu ya namna walivyotoweka wasichana hao.
Hali ya usalama ni mbaya sana huku miundo mbinu duni ikichangia kuifanya hali ngumu kuweza kufikia maficho ya kundi hilo na pia kubaini idadi ya wasichana waliotoroka kutoka mikononi mwa Boko Haram.
BBC imeongea na jamaa ya wasichana watatu ambao walitoroka. Sasa wako salama nyumbani kwao na mmoja wao amesema kwamba wasichana wengi wamefanikiwa kutoroka.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa huenda wasichana hao walitoroka siku ya Ijumaa, pale watekaji nyara walipokwenda kushamblia kambi ya kijeshi.
Maafisa wakuu hata hivyo bado hawajaweza kuthibitisha kutoroka kwa wasichana hao.
Wakati huo huo hapajakuwa na taarifa zozote kuhusu wasichana 200 waliotekwa nyara katika shule ye bweni ya Chibok mwezi Aprili. Jambo ambalo limekemewa vikali na jamii ya kimataifa huku baadhi ya mataifa kama vile Marekani, Uingereza na hata Ufaransa wakijitolea kuisaidia serikali ya Nigeria kuwasaka wasichana hao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni