Watu
wawili wameripotiwa kuuawa baada ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi
kufuatia ghasia kati ya polisi na waandamanaji katika mji mkuu wa
Bujumbura nchini Burundi.
Waandamanaji wameishutumu serikali kwa
kufanya mapinduzi ya kikatiba baada ya uteuzi wa rais Pierre Nkurunziza
kupigania muhula wa tatu,Mwandishi wa BBC anasema kuwa watu wengi wamejeruhiwa huku wengine wakikamatwa.
Maafisa wa polisi walikivamia kituo kimoja cha redio kinachounga mkono upinzani na kutishia kukifunga iwapo hakitasitisha matangazo yake ya moja kwa moja kuhusu maandamano hayo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni